Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera limepitisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya Mapato ya kiasi cha Sh. 66.6 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ya halmashauri hiyo.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Chrisant Kamugisha amewasihi wataalamu kufanyakazi kwa weledi ili kuhakikisha mpango na bajeti iliyopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani mapato yanakusanywa kwa asilimia 100 na hata kuvuka malengo.
 
Amesema kuwa katika Mchanganuo wa mapato hayo Mapato ya ndani yatakuwa Sh 3,66 bilioni , ruzuku ya Matumizi ya Halmashauri Sh1.76 bilioni ruzuku ya Mishahara Sh51.43 bilioni na ruzuku ya Miradi ya Maendeleo Sh9.75 bilioni.
 
“Tukizingatia mgawanyo wa fedha hizo asilimia 40 itatekeleza miradi ya maendeleo na asilimia 60 itatumika kwenye matumizi mengineyo hivyo watendaji wetu na wakusanyaji mapato wafanye kazi kwa uadilifu tuwapatie wananchi huduma bora za jamii,” amesema Kamugisha.
 
Aidha, baadhi ya madiwani waliochangia bajeti hiyo wamemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo na wakuu wa idara kukamilisha miradi viporo katika sekta ya maji, elimu afya na barabara kuharakisha huduma lakini pia kuwachukulia hatua wasiotimiza wajibu wao kiutumishi.
 
  • Uwindaji panya waharibu misitu
 
  • Tanzania ya zamani ilikuwa ikiishi kama nchi yenye Laana- Askofu Kakobe
 
  • Video: Walimu wabovu waziponza shule za Umma
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi, Richard Ruyango amesisitiza juu ya uwajibikaji kulingana na malengo yaliyopangwa, udhibiti wa Uvuvi haramu na kupongeza juu ya ukusanyaji wa mapato uliovuka malengo kwa mwaka wa fedha ulioisha 2017/2018

Mradi wa TACIP wazidi kuwafikia wasanii nchini, RC Kebwe aupa tano
Kangi Lugola awakuna Watetezi wa haki za binadamu