Mume  wa mwanadada Amber Rutty, anayefahamika kwa jina la Devil amedondoka na kupoteza fahamu leo alipokuwa mahakamani ambapo walifika kwa ajili ya kusikiliza kesi yao inayoendelea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Januari 10.

Mwanadada huyo na mume wake ambao wamefunga ndoa siku chache zilizopita walipata skendo ya kuvujisha video wakifanya mapenzi kinyume na maumbile na kusweka lumande kwa muda kidogo mpaka pale walipopata dhamana.

Amber Rutty amesema kuwa sababu kubwa ya mume wake kudondoka mahakamani hapo ni kutokana na ukweli kuwa hakuwa na hali nzuri kwa muda mrefu tangu ametoka selo mara ya mwisho.

”Hali yake haikuwa nzuri tangu tulipota rumande, wote tuliondoka na magonjwa lakini mwenzangu hakuwa vizuri zaidi, lakini namshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri”. Amesema Rutty.

Hata hivyo Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Februari 12, mwaka huu wa 2019.

 

Video: Zitto Kabwe kuburuzwa mahakamani
Picha: Huddah atimba mtaani na buibui kusaka matapeli

Comments

comments