Mhadhiri wa chuo kikuu cha ardhi, Dkt. Job Asheri Chaula ambaye pia ni mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Jennifer Mgendi amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na uongozi wa Chuo hicho na kusema kuwa Dkt. Chaula alikuwa Mkuu wa ‘School of Earth Sciences, Real Estate, Business and Informatics (SERBI)’.

Chuo kimesema taarifa za mazishi zitatolewa mipango itakapokamilika. Dkt. Chaula ameacha mke na watoto watatu

Waziri Kabudi akabidhiwa dawa ya Corona kutoka Madagascar
Corona Senegal: watoto wa mtaani 2,000 waokolewa