Msanii wa nyimbo za Injili Rose Alphonce Nungu maarufu kama Muna Love amelaumiwa vikali na ndugu yake wa karibu kutokana na tabia yake ya kumpotezea mwanaye wa kumzaa ambaye hafahamiki katika mitandao ya kijamii.

Ndugu wa Muna Love alihojiwa na kusema ifike kipindi Muna aache maisha ya kuigiza na kuishi maisha yake ya kweli kwani amekuwa akisaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kumuacha mtoto wake wa kumzaa akitaabika na kulelewa na watu wengine.

Muna ambaye siki za hivi karibuni alipatwa na msiba mkubwa wa kufiwa na mtoto wake Patrick amejikuta akiokoka na kusema maisha ya mwanaye yamembadilisha kwa kiasi kikubwa na kumfanya atafute wokovu.

Muna amekuwa akinukuliwa akisema kuwa Patrick ndiye mtoto wake wa pekee, lakini nyuma yake kuna madai kuwa alizaa mtoto mmoja wa kiume (jina linahifadhiwa kimaadili) mwenye umri wa miaka 13.

”Tunashangaa sana Muna huwa hamtambulishi kabisa mtoto wake mkubwa na nasikia alisema aliwahi kuzaa mtoto akafa wakati mtoto yupo hai na anatakiwa apate upendo kutoka kwa mama yake.

”Kinachouma ni kwamba Muna sijui ataishi maisha ya kuigiza mpaka lini ilihali anawasaidia watoto wenye matatizo, hatukatai ni wajibu yeye kusaidia, lakini amwangalie na mtoto wake ambaye alimtoa katika tumbo lake. “Mtoto huwa anawaambia wenzake shuleni kuwa mama yake mzazi ni Muna na wenzake wanamwambia mbona hawajawahi kumuona akija kumwangalia? Mtoto anaishia kulia tu” alizungumza ndugu wa Muna wakati akifanyiwa mahojiano.

Aidha, Muna alitafutwa ili kuthibitisha taarifa hizo, alikanusha na kusema hazina ukweli wowote.

 

Chadema kutafakari kumpa Maalim Seif kuwania Urais
Burundi kikaangoni kwa kuitimua timu ya UN

Comments

comments