Muna amesema kuwa amepitiwa na shetani hadi kufikia hatua ya kusema msiba wa mtoto wake Patrick ufanyike nyumbani kwake Mbezi na kuandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa Peter ambaye ametangaza kuwa Patrick ni mtoto huyo wake, siyo kweli.

Muna amesema “Najua nimekosea ndio maana posti yangu nimeifuta niliyoiandika jana kuwa mtoto sio wa Peter, shetani alinipitia, hivyo msiba utakuwa Mwananyamala kwa Peter na sio Mbezi kama nilivyosema hapo mwanzo,”.

Sekeseke hilo limeibuka kufuatia sintofahamu kuhusu nani ni baba halisi wa mtoto wa Muna, Patrick na wapi msiba upelekwe hatimaye Muna amekubali msiba upelekwe kwa baba wa mtoto huyo, Peter Zacharia Komu, maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Awali, Muna kupitia ukusara wa mtandao wa kijamii wa Instagram aliandika baba wa mtoto ni Casto Dickson, huku akisisitiza msiba utafanyika nyumbani kwake Mbezi, huku akimtaka Peter aache kuongea maneno kwani anasiri nzito moyoni.

Naye Eve ambaye ni dada yake Muna amesema kuwa ni kweli Muna amekubali msiba uwe nyumbani kwa Peter, sababu ndiyo baba halali wa Patrick.

“Tunamshukuru Mungu tena sana, kweli Muna amekubali msiba uwe Mwananyamala kwa mume wake, na hivi wako ubalozini wanafanya mchakato wa kuuleta mwili kesho Tanzania.” Amesema.

Mtoto Patrick alifariki dunia Julai 3, 2018 Nairobi, nchini Kenya alikokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake unatarajia kuletwa Tanzania kesho Julai 6, 2018 na maziko yatakuwa Jumamosi.   

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 6, 2018
Polepole akanusha CCM kumlima barua ya onyo Nape

Comments

comments