Mama mzazi wa marehemu Patrick, Muna Love amemshukuru Mungu kwa kila jambo ambalo amelipitia kwani anaamini kila kitu kinachotokea duniani ni mipango ya Mungu na daima Mungu huwa nyuma ya jaribu lolote ambalo binadamu anakumbana nalo.

Aidha, Muna amesema kuwa pale Mungu anapokujaribu haimaanishi kuwa hakupendi au anataka kukuumiza hapana, ila Mungu hutoa jaribu kuimarisha na kamwe hawezi kukuacha.

Kupitia akaunti yake ya instagram ametoa ujumbe huo mzuri wenye kutia moyo hasa kwa wale ambao wanapitia magumu na kuhisi Mungu hayupo nao, Ameandika.

“Mungu anawapenda watu wote bila kujali wewe ni nani na unatabia gani mbele zake …na atatumia njia anazojua ili zikufikie na umtambue urudi kwake ukazaliwe upya… na hata pale anakupa jaribu sio kama hakupendi au anataka akuumize hapana, anakupa jaribu na pia anajua utaliweza na hatoweza kukuacha kamwe atakupa na njia za kupita.

“Mungu kwenye kila jaribu lile la aina yoyote jua yupo nyuma yako na anakukomaza ili kumuonyesha shetani kua wewe ni mtoto wake na anajivunia wewe sasa ,usiwaze kumuhukumu Mungu au kuumia kwanini umepitia hilo bali mshangilie na kumtukuza uone matunda atakayokupa 🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽

“Asikudanganye mtu Mungu awezi kukuacha upitie gumu bila kukupa njia na roho mtakatifu akakuongoza asante Mungu wangu nitakutumikia milele,” amesema Muna.

Aidha, siku chache zilizopita Muna alifanya mkutano na vyombo vya habari kuelezea kinagaubaga jinsi safari ya mwanae Patrick mpaka kupoteza maisha, pia aliweka wazi juu ya suala la baba mtoto wa Patrick lililoibua sintofahamu wakati msiba wa mtoto huyo ukiwa unaendelea, hivyo Muna alifunguka na kusema mtoto ni wa Patrick hali iliyovunja sintofahamu hiyo.

Simiyu: Tunaweza vipi kusema NASA bado ipo?
Arsenal yamuweka njia panda Aaron Ramsey

Comments

comments