Muongozaji na muaandaji mkongwe wa filamu nchini Marekani John Singleton amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa  na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu.

John mwenye umri wa miaka 51 alikuwa kwenye ‘life support’ kwa siku kadhaa katika chumba cha uangalizi wagomjwa mahututi mjini Los Angeles.

Familia yake imethibitisha kifo chake baada ya kuondolewa kwenye mashine hiyo usiku wa kuamikia leo.

Muongozaji huyo nguli aliingia kwenye historia ya kuwa mtu mweusi wa kwanza mwenye umri mdogo (24) na kuwa nominatedi kwenye tuzo kubwa za filamu za Academy Award.

Hata hivyo Umaarufu wake ulibebwa na filamu kubwa ambayo alioongoza  mwaka 1991 Boyz N the Hood iliyowakutanisha wakali kama Ice Cube, Nia Long na wengine.

 

Waziri Mkuu ahimiza wakazi wa Dodoma wachangie damu
TANESCO Njombe waahidi kutatua tatizo la umeme Vijijini