Siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kukabidhiwa orodha ya majina ya vigogo ambao baadhi ni viongozi wa Kanisa la Baptist wanaotuhumiwa kutumia vibaya fedha za Chuo Kikuu cha Mount Meru kiasi cha Bilioni 3 tayari kazi ya kuwatafuta imeanza na tayari aliyekuwa mkuu wa kwanza wa chuo hicho, Harrison Olan’g amekamatwa na Jeshi Polisi Wilayani Arumeru kwa ajili ya mahojiano.

Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wa kwanza, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema wao walipokea maombi kutoka kwa mwangalizi mkuu wa Kanisa la Baptist Tanzania Mchungaji, Arnold Manase kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wote wa ubadhirifu wa mali za Chuo Kikuu cha Kanisa la Baptist cha Mount Meru ambao wanatuhumiwa kuhujumu zaidi ya Shilingi Bilioni 3,  hatua iliyosababisha chuo kushindwa kujiendesha na hatimaye kufungiwa na TCU.

Aidha, Muro amesema wao kama Serikali wanatekeleza ombi la Kanisa la kuomba kuingilia kati sakata hilo ili haki itendeke na kusisitiza kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa jeshi la Polisi kuendelea kuwasaka watuhumiwa wengine na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili haki itendeke.

“Kazi inaendelea, tunaomba ushirikiano wa wananchi katika kuwabaini wengine” amesema Muro.

 

Revocatus Kuuli afungiwa maisha, Young Africans kuchaguana Januari 13
Wanaume waongoza kwa kujiua