Wakati Haji Manara akitupa dongo katika klabu ya Young Africans, haikuchukua hata saa 24, jibu kutoka kwa mpinzani wake Jerry Muro likapatikana tena ikiwa ni baada ya ushindi wao wa mabao mawili kwa moja dhidi ya APR, pale jijini Kigali nchini Rwanda.

Muro amejibu hoja za Manara, kwa kumtaka ajisifie yeye mwenywe, na si kuangalia kina nani waliwahi kufanya makubwa na mangapi katika klabu anayoitumikia kwa sasa.

Ujumbe wa Muro Kwa Manara nao ulisambazwa katika mitandao ya kijamii kama ilivyo ule uliotuma kwao.

Ujumbe wa Jerry Muro ndio huu:-

Haikatazwi mtu kujivunia historia zilizowekwa na watangulizi wetu,mfano hayati baba wa taifa mwalimu nyerere na wengine wengi tu Tanzania, Africa na dunia, wao walitimiza wajibu wao ndio mana leo tunawaota na kuwaimba na kuwasifu.

Lakini ni jambo jema na zuri la kujivunia ni historia inayowekwa na mtu mwenyewe, mfano mimi Jerry Cornel Muro, najivunia kuweka historia ifuatayo kwenye ulimwengu wa soka:-

  1. Nimemfunga simba mara mbili mfululizo ukiwa ni ushindi pacha mujarabu goli 2:0 round ya kwanza na 2:0 round ya pili katija msimu huu wa ligi hii haijawai kutokea katika historia ya dunia tangu kuumbwa kwake mimi nikiwa miongoni mwa viongozi wakuu kabisa wa klabu ya Yanga na haitatokea historia kama hii tena katika ulimwengu.
  2. Nimefanikiwa kuweka historia ya kuzifunga timu kubwa za kikataifa BDF, PLATNUM FC, CERCLE DE JOACHIM, APR na zingine nyingi tu, kwangu mimi ni mafanikio makubwa sana katika maisha yangu.
  3. Najivunia kuwa mbunifu wa kwanza kuanzisha uwepo wa mfumo wa idara kubwa ya habari na mawasiliano Yanga mfumo ambao tangu nimeuanzisha umeonekana kupendeza na kuwavutia wengi ambao wameigia mfano simba, hawajai kuwa na huu muundo wameiga kwetu sisi Yanga wabishe na hili, ulimwengu unajua, africa inajua na Tanzania inajua najivunia kuwa mwanzisha mwendo wa idara ya habari katika soka la Tanzania japo wanaoiga hawana standards and qualification za huu muundo.
  4. Najivunia kunyakua kombe la ubingwa wa ligi kuu nchini Tanzania msimu uliopita nikiwa ndio nimeanza kazi Yanga.
  5. Najivunia kunyakua Ngao ya jamii katika msimu huu wa ligi nikiwa kiongozi wa Yanga.
  6. Najivunia kuwa kinara wa utoaji wa majina dhahania kwa

wapinzani wangu wa jadi

-wamchanganu

-wa matopenii

-siku zote kisigino hakikai mbele.

-ikiwaka mulika ikizimika…….

Najivunia huu ubunifu watu sasa wanapa ladha ya burudani za kimichezo zilizojaa tambo za uhakika.

  1. Najivunia kumliza mtani wangu jamaa mmoja hivi ambae alikuwa anajisemea kimoyoni japo watu walisikia kuwa tangu amezaliwa hajawai kukutana na changamoto kubwa katika maisha yako kama anayokutana nayo sasa hivi kutoka kwangu, anaomba ardhi ipasuka nitoweka uku kwenye soka.

 

Ndugu zangu mafanikio yako mengi sana ambayo nikianza kuyataja yanaweza kufika mpaka mtaa wa msimbazi na aggrey nisiwachoshe sana kusoma huu waraka.

Nimalize kwa kusema tu ni jambo jema kujivunia historia za wenzako, lakini ni jambo la heshima sana kujivunia historia yako unapopata fursa ya kuongoza au kusimamia jambo au kitu uku duniani, hata kuisimamia familia yako ikapata mafanikio nayo ni historia.

Wenu katika michezo

Jerry Cornel Muro

Kigali, Rwanda

Azam FC: Tutapambana Hadi Dakika Ya Mwisho Vs Bidvest
Anne Malecela aeleza sababu za ‘kulikuna’ jicho la Magufuli