Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa anampenda rais wa Marekani, Donald Trump kwa misimamo yake anayoionyesha.

Ameyasema hayo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala. ambapo amesema Marekani ina Rais mzuri anayesimamia kile anachokiamini.

”Ninampenda trump kwasababu anasema ukweli mtupu, waafrika wanatakiwa kusuluhisha matatizo yao wenyewe, Waafrika ni dhaifu sana,” amesema Museveni

Aidha, Pongezi hizo za Museven kwa Trump zimekuja muda mfupi mara baada ya balozi wa Uganda kwa Marekani Deborah Malac kumkosoa Trump.

Hata hivyo, Mapema mwezi huu Trump alidaiwa kutoa kauli za kejeli juu ya nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya wahamiaji.

Daktari atoa ripoti ya ukichaa wa ‘nabii Tito’
Obasanjo amtaka Buhari kupumzika masuala ya siasa