Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anatarajiwa kuanza kuongoza mkutano wa kutafuta usuluhishi wa mgogoro na kutafuta amani nchini Burundi utakaoanza kesho jijini Kampala.

Museveni aliteuliwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongoza mazungumzo hayo ili kupata muafaka wa kisiasa kufuatia mauaji ya mamia ya wananchi yanayoendelea nchini humo.

Hali ya amani imetoweka nchini Burundi baada ya rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza kuongeza muhula mmoja wa kukaa madarakani kuwa mihula mitatu, kinyume cha katiba na mazungumzo ya amani ya Arusha yanayoweka ukomo wa mihula miwili ya urais nchini Burundi.

Mazungumzo hayo yanayoanza kesho yanatarajiwa kuyakutanisha makundi 14 yanayowakilisha maslahi mbalimbali ya wananchi wa Burundi.

Waziri wa ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga aliiambia BBC kuwa baada ya mazungumzo hayo kuzinduliwa jijini Kampala, yatahamishiwa jijini Arusha, Tanzania ambapo chama tawala cha Burundi cha CNDD – FDD pamoja na mengi yanayompinga Nkurunzinza watahudhuria.

 

BEN POL AELEZA KILICHOPELEKEA ‘AVRIL’ KUTOONEKANA KWENYE VIDEO YA 'NINGEFANYAJE
Dk. Slaa Amrudia Tena Gwajima