Rais wa Uganda’ Yoweri Museveni amesema bado anaangalia ni chanjo ipi atakayochomwa, siku chache baada serikali yake kuanza kutoa chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa wananchi.

Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo, Rais Museveni amesema hajapata chanjo bado kwa kuwa yuko makini na ana ulinzi wa kutosha “.

Aidha amebainisha kuwa mke wake, Janet Museveni, pia bado hajapata chanjo hiyo.

“Bado naangalia nipate chanjo ipi, ile ya Johnson&Johnson, ile ya Uchina au ya Urusi. Ya kwetu ya Uganda itakuja pia huenda ikatumika baadae sana,” amesema Museveni.

Wachezaji AS Vita watangaziwa ahadi nzito
CAF: Agab, Bakhit ruhsa kucheza Al Merrikh