Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa hakuna uasi wa vijijini wala ugaidi wa mijini utakaofanikiwa. Amesema hayo kufuatia mashambulizi mawili tofauti ya mabomu nchini humo mwezi huu.

Katika hotuba yake ya televisheni kwa umma, Museveni amewataja wahalifu hao kuwa ni kupe wanaoshambulia raia wasio na silaha, ambao watasakwa na kutiwa nguvuni.

Kundi la ADF linalojinasabisha na kundi la kiislamu la IS linalaumiwa kwa mashambulizi hayo mawili.

IS limekiri kuhusika na shambulio liliotokea Oktoba 23, katika mji wa Kampala na kusababisha kifo cha muhudumu mmoja wa baa na kujeruhi watu wengine watatu.

Mlipuko mwingine kwenye basi lilokuwa linatoka Kampala kwenda magharibi mwa nchi hiyo ulitokea Okrtoba 25, na kwa mujibu wa Polisi mlipuko huo ulimuua mlipuaji wa kujitoa mhanga , aliyekuwa amelivaa bomu hilo.

Kundi la ADF lina historia ya kuendesha vitendo vya kigaidi mijini na kwa mujibu wa Rais Museveni, walihusika kwenye ulipuaji wa mabomu 30 mjini Kampala kati ya mwaka 1997 na 2001, na kuua zaidi ya watu 120.

Tshisekedi atuhumiwa na Ubaguzi Israel
Mjumbe Maalum UN awakingia kifua Zimbambwe