Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya MTN ambayo imekuwa ikifanya biashara zake nchini Uganda ameruhusiwa kurejea nchini humo na anatarajiwa kuwasili Kampala.

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MTN ya nchini Uganda, Wim Vanhelleputte alifukuzwa kutoka nchini humo Februari 15, 2019, kwa sababu za usalama wa taifa, polisi walisema wakati huo, bila ya kutoa maelezo zaidi.

“Tumejulishwa rasmi, tumepata barua na ilikuwa ni rais ndiye alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kutuandikia na kumruhusu mtendaji wa MTN kurejea haraka nchini na hivyo atawasili hivi leo,” amesema mwenyekiti wa MTN Uganda, Charles Mbire.

Amesema Vanhelleputte huenda akaanza shughuli zake kama mkuu wa kampuni.

Hata hivyo, amesema kuwa maendeleo hayo ni dalili ya kwanza ya kurejea kwa uhusiano mwema kati ya kampuni na serikali ya rais, Yoweri Museveni, kufuatia shutuma kuwa mtandao wa kampuni ulijihusisha na shughuli za kijasusi na kukwepa kodi na miongoni mwa masuala mengine.

R Kelly akabiliwa na Mashtaka mapya 11
Mama mjamzito ajipasua, amtoa mtoto