Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza Baraza lake la Mawaziri mapema wiki hii likiwa na idadi ya Mawaziri 50 na mmoja kati yao ni mkewe, Janet Museveni.

Museveni amempa mkewe usimamizi wa Wizara muhimu ya Elimu na Michezo ikiwa ni miezi michache baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kuhalalisha ushindi wake katika uchaguzi mkuu uliomalizika mwaka huu ambao ulipingwa Mahakamani na Mpinzani wake, Amama Mbabazi.

Uteuzi huo umezua gumzo kwani hivi karibuni Rais Museveni alimpandisha cheo mtoto wake Jeshini, hali inayotafsiriwa na wakosoaji wake kama upendeleo wa kifamilia.

 

Wanafunzi kuhukumiwa hadi miaka 10 jela kwa kuharibu picha ya Rais
Lema: Sishangai Waziri kuingia Bungeni Amelewa wakati kulikuwa na bar ndani ya uzio wa bunge