Wakati wananchi wa Uganda wanatarajia kupiga kura kesho, Rais Yoweri Museveni ambaye pia ni miongoni mwa wagombea, amemuonya mpinzani wake mkuu Dk. Kiza Besigye kutojaribu kuwa na kituo cha kujumlisha kura zake.

Akiwahutubia wafuasi wa chama chake cha NRM jana, Museveni amesema kuwa kazi ya kujumlisha kura ni ya Tume ya Uchaguzi na kwamba Besigye akijaribu kuwa na ‘Tally Center’ atakamatwa na kufungwa jela.

Musevini kampeni

Rais Yoweri Museveni akipokelewa na wafuasi wake

“Besigye anapaswa kufahamu kuwa nchi hii inaongozwa na watu ambao walipigana vitani. Kama ataendelea na mpango wake wa kuwa na vituo vya kujumlisha kura kama Tume, ataishia kufungwa jela,” alisema Museveni.

Museveni alitoa tamko hilo wakati ambapo wapinzani wake wakipinga agizo la Tume ya Uchaguzi kuwataka wagombea wasiende na simu za mikononi wala kamera katika vituo vya kuhesabia kura. Wagombea hao walidai kuwa hakuna sheria inayozuia vitu hivyo.

Mbinu ya kuwa na kituo cha kujumlishia matokeo iliwahi kutumiwa na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa nchini Tanzania wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25. Hata hivyo, vyama hivyo vilieza kuwa vijana waliokuwa wanafanya kazi hiyo walitiwa mbaroni katika eneo la Sinza jijini Dar es Salaam na vifaa vyao kuchukuliwa.

Admin wa Facebook akamatwa kwa kuandika haya kuhusu wake za watu
Mimba ya Wema Sepetu yayeyuka, Idris alia kupoteza mapacha