Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaonya wananchi wa Uganda dhidi ya vitendo vya kutumia mdomo katika kufanya mapenzi akidai kuwa mdomo umeumbwa kwa ajili ya kula na si mapenzi.

Museveni amesema kuwa utamaduni huo wa kutumia mdomo katika mapenzi uliletwa na wageni.

”Nichukue nafasi hii kuonya watu wetu hadharani dhidi ya vitendo visivyo sahihi vilivyoletwa na vinavyoendelezwa na wageni. Mojawapo ni mapenzi ya kutumia mdomo. Mdomo ni kwa ajili ya kula si mapenzi”.

Museveni amezungumza hayo wiki iliyopita wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.

Na vyombo vya habari vimeripoti onyo hilo na kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, ambako baadhi ya watu wanapingana naye na wengine kumpongeza.

Kauli yake ilitoka siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonysha ofisa mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Makerere akipigana busu mdomoni na mwanamke ofisini kwake.

 

TCRA yatoa siku 14 za usajili wa huduma mtandaoni
Serikali kuwapima wanaume Ukimwi bar kwa bar

Comments

comments