Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni, ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima juhudi zozote za kuzua ghasia baada ya kuchaguliwa kwake tena. 

Museveni amewaambia wanahabari katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura nje ya mji mkuu Kampala kwamba hakuna atakayezua ghasia katika eneo hilo kwa sababu yeyote atakayejaribu kufanya hivyo atakabiliwa vilivyo. 

Katika taarifa, jeshi la polisi nchini Uganda limesema kuwa limewakamata takriban watu 84 kuhusiana na ghasia za uchaguzi.

Lakini kupitia televisheni ya taifa, msemaji wa chama cha NUP Joel Ssenyonyi amesema kuwa maafisa wa usalama walikuwa wakiwatesa kwa utaratibu washirika wa upinzani.

Makazi ya Wine, msanii aliyegeuka kuwa mwanasiasa yaliyoko kwenye mji mkuu, Kampala yamezingirwa na wanajeshi tangu Ijumaa jioni na kumfanya kuwa chini ya kifungo cha nyumbani.

Mapema jana, tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza Museveni mshindi wa uchaguzi huo wa rais baada ya kupata kura milioni 5.85 huku mpinzani wake wa karibu Wine akipata kura milioni 3.47.  

 Duddridge amesema kuwa ni muhimu kwa wasiwasi huo kuelezwa, kuchunguzwa na kutatuliwa wa njia ya amani, kisheria na kikatiba. Marekani kwa upande wake imeelezea wasiwasi kuhusu taarifa za ghasia na dosari zilizojitokeza katika uchaguzi huo mkuu wa Uganda.

Nyama ya kitimoto yapigwa marufuku
Biden kusaini maaagizo 12 ya urais