Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewashukia wapinzani wake kwa kubeza kila juhudi anazozifanya kuwaletea wananchi wa nchi hiyo maendeleo.

Museveni ambaye pia ni kiongozi wa chama tawala cha NRM, jana alieleza namna ambavyo serikali ya chama hicho imekuwa ya vitendo zaidi baada ya kuweka umeme katika eneo la Lalogi na kuwataka upande wa upinzani wanaobeza juhudi hizo kushika nyaya za umeme zilizopo hapo ili wathibitishe.

“Watu wa upinzani wanaosema hatujafanya kitu wanapaswa kuja na kugusa hizi nyaya za umeme kwa ajili ya kuthibitisha,” Rais Museven alitweet.


Katika hatua nyingine, Museveni aliwataka wananchi kutoamini kile ambacho kimekuwa kikielezwa na wapinzani wake kuwa Serikali yake iko mbioni kufanya mabadiliko kwenye katiba ili kuwasaidia kuiba ardhi.

Crystal Palace Yakubali Kumsajili Christian Benteke
Serikali Yawataka Watendaji Kupanda Miti Hekta 185,000 Kwa Mwaka