Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amezindua kitengo kipya cha kupambana na rushwa na Ufisadi nchini humo na hasa katika idara zote za Serikali kuchunguza tatizo la rushwa.

Amesema kuwa jukumu la kupambana na rushwa liko kwa wananchi, ambapo amewataka kuwasiliana na kitengo hicho kipya kitakachohudumu moja kwa moja chini ya ofisi yake.

Museveni yupo katika shinikizo la kuonyesha uwajibikaji wa serikali yake, huku akikabiliwa na changamoto ya upinzani kutoka kwa wanasiasa wanaowavutia wapiga kura vijana kama mwanamuziki na mbunge Bobi Wine.

Katika hatua nyingine, Museveni ameeleza kwamba kiongozi anayekabiliwa na tuhuma za rushwa, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Sam Kutesa anachunguzwa kwa tuhuma za kula rushwa ya thamani ya dola nusu milioni kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa Hong Kong.

Hata hivyo, Uganda imeorodheshwa kuwa katika nafasi ya 151 kati ya mataifa 180 yaliochunguzwa kwa rushwa katika ripoti ya Februari mwaka huu ya shirika la Transparency International.

Mafuriko ya wasafiri, Wamiliki wa Mabasi waililia Serikali
Rais Magufuli aendelea kuwabana mbavu TRA