Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameripotiwa kufanya mazungumzo na kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini humo, kufuatia sakata la madai ya kuwa kiongozi huyo amepanga kuipindua Serikali.

Taarifa za Ikulu zimeeleza kuwa Rais Museveni na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kampala, Cyprian Kizito Lwanga walizungumza kwa njia ya simu Jumatatu wiki hii.

Mazungumzo kati ya wawili yamefanyika siku chache baada ya Askofu Kizito kueleza kuwa alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu ambaye alimuonya kuwa anafahamu kile alichokiita njama anazozisuka kwa lengo la kuipindua Serikali.

Askofu Kizito aliweka wazi vitisho hivyo alivyovipokea alipokuwa akiongoza ibada ya Siku Kuu ya Pasaka katikaka viwanja vya kanisa hilo vilivyoko Rubaga.

Ikulu ya Uganda imeeleza kuwa sakata hilo litajadiliwa na viongozi hao na ufumbuzi utakaopatikana utawekwa wazi.

Gavana atuhumiwa kwa ubakaji
Canelo ajiengua pambano lake na Golovkin