Kocha Mkuu wa Ligi ya Mabingwa Wanawake Tanzania Bara Simba Queens Mussa Hassan Mgosi, ametoa ufafanuzi wa mchezaji mpya ndani kikosi chake ambaye ameushtua umma wa wapenda soka nchini.

Mchezaji huyo anayefahamikaa kwa jina la Victoria alionekana kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Simba SC jana Jumanne (Julai 13), wakati wa mchezo wa Kirafiki dhidi ya Twiga Stars, Uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Mgosi ametoa ufafanuzi wa mchezaji huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii (Facebook) kwa kuandika: “Naomba niliweke sawa kuhusu mchezaji Victoria ni mtanzania anasoma Marekani yupo Tanzania kwa likizo ya shule hivyo kaja kwa wazazi wake Tanzania.”

“Anasoma Marekani na anacheza mpira hivyo waliomuona walinifikishia ujumbe na videos zake na picha hivyo nilihitaji nione kipaji chake ndio mana nilimpa dk 10 lakini hayupo kwenye usajili wa Simba Queens”

“Hivyo shule zikifunguliwa atarudi Marekani na kuitangaza Simba kwa wanafunzi WENZIE huko maana kila mmoja anapost Simba imemsajili mmarekani msipotoshe uma na ni vyema kuuliza ili kujua Simba ni team kubwa na inampa nafasi kipindi muafaka mchezaji yeyote kuja kuonesha alicho nacho nadhani tutakuwa tumeelewa kuhuhusu mmarekani.”

Simba Queens inayojiandaa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati itakayofanyika nchini Kenya baadae mwezi huu, iliopoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Twiga Stars kwa mabao 2-1.

Wachezaji wa Simba Queens wakifuri baada ya kukabidhiwa Kombe la Ubingwa la Ligi Kuu 2020-21.

Hata hivyo baada ya mchezo huo Simba Queens walikabidhiwa Kombe la Ubingwa la Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2020/21.

Niyonzima: Naachana na Young Africans, Siachi mpira
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 14, 2021