Meneja wa klabu ya Inter Milan Roberto Mancini, hii leo anatarajiwa kukutana na mmiliki wa klabu hiyo kwa ajili ya kufahamu mustakabali wa kuendelea kubaki Giuseppe Meazza.

Kikao cha meneja huyo kutoka nchini Italia pamoja na mabosi wake, kinatarajiwa kuwa na mzungumzo ya muda mrefu, kutokana na tetesi zilizoibuka siku za hivi karibuni ambapo ilidaiwa Mancini huenda akaamua kuachana na The Nerazzurri, kutokana na kuchoshwa na baadhi ya mambo yanayoendelea klabuni hapo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika gazeti la michezo la nchini Italia (Gazzetta dello Sport), kumekua na mahusiano yasiyoridhishwa baina ya pande hizo mbili.

Jambo kubwa ambalo linatajwa kumkera Mancini, ni kutopendezwa na mwenendo wa usajili wa wachezaji klabuni hapo, ambapo mpaka sasa hajakamilishiwa mpango wa kufanya usajili wa aliowapendekeza kwa ajili ya maboresho ya msimu ujao wa ligi ya nchini Italia, ambayo itaanza rasmi mwezi ujao.

Hata hivyo kama itatokea Mancini, anatangaza kujiuzulu nafasi yake atapata hasara ya kupoteza kiasi cha Euro milion 5 kwa kila mwaka ambao umesalia kwenye mkataba wake.

Gabigol Akwamisha Makubaliano Ya Santos FC Na Juventus FC
Zimebaki Saa 24 Kwa Gonzalo Higuain