Mbunge wa Geita Vijijini ,Joseph Kasheku Musukuma, wakati akitoa mchango wake katika Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2021/2021 amempongeza Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa kupunguza tozo kwa madereva bodaboda katika bajeti yake aliyoisoma ambapo moja ya Mapendekezo katika bajeti ni punguzo la faini kwa dereva bodaboda na bajaji.

Ameyasema hayo leo Juni 14, 2021, Bungeni Dodoma, ambapo leo abunge wameanza kuchangia maoni yao katika Bajeti Kuu ya serikali ya mwaka 2021/2021, iliyosomwa Bungeni Juni 11, 2021, na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.

“Waziri nakupongeza sana kwenye faini ya bodaboda, nataka nikuambie katika kitu ambacho Mungu atakukumbuka na kukuongezea hata siku zako za uhai wako ni suala la faini ya bodaboda, unajua mimi nilikuwa najiuliza wachumi wetu mko namna gani, mimi nilikuwa najiuliza inawezekanaje faini ya bodaboda anayebeba watu wawili unalinganisha na faini ya basi la watu 65?, mimi nilikuwa nashauri hata hiyo 10,000 bado ni nyingi tungeweka hata 2000,” amesema Mbunge Musukuma.

TANZIA: Mfanyabiashara mkubwa Kenya Chris Kirubi afariki dunia
Mwanaume mwenye familia kubwa zaidi duniani afariki dunia