Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema Jeshi hilo limemkamata Dezber Kahwa (49) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Mwanafunzi wa Darasa la Sita kwa kumtoa mimba kwa njia za kienyeji.

Kamanda Malimi ameeleza kuwa, baada ya Uchunguzi, imegundulika kuwa chanzo cha kifo cha Mwanafunzi huyo wa miaka 14 ni kutobolewa kwa mfuko wa uzazi na kuingizwa dawa yenye sumu.

Alisema kuwa muuguzi huyo alifukuzwa kazi wakati wa zoezi la kuhakiki vyeti feki, baada ya kugundulika kuwa hana Cheti cha Kidato cha Nne. Hata hivyo, aliendelea kuhudumia mtaani pasipo kuwa na kibali.

”Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na Polisi lakini tayari mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari wa binadamu katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Kagera na uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni kutobolewa kwa mfuko wa uzazi na kuingizwa dawa sumu” amesema Malimi.

Aidha Kamanda Malima amesema kuwa baada ya jaribio hilo binti huyo alipata maumivu ya tumbo na kwenda na kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa amabko inadaiwa alipatiwa matibabu ya maumivu ya tumbo, kitendo ambacho ndugu na jamaa wanahisi ndiyo sababu ya kifo chake.

Tanzia: Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda afariki dunia
TMA: Tahadhari ya mvua kubwa kwa siku tano

Comments

comments