Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Peter Muiya Irungu anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuiba sadaka katika Kanisa Kuu la James lililopo Murang’a nchini Kenya.

Inadaiwa kuwa Mtuhumiwa huyo hujifanya anasali na watu wote wanapoondoka Kanisani, anafungua masanduku ya sadaka kwa kutumia waya maalumu.

Uongozi wa Kanisa hilo uliamua kuweka kamera za siri baada ya sadaka kuanza kupotea.

Kanisa hilo limesema limeshangazwa na kitendo hicho cha Irungu, kwakuwa ni mmoja kati ya waumini wenye mahudhurio mazuri Kanisani na hajawahi kukosa ibada hata siku moja.

Aidha, watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyo wanasema alianza tabia za wizi tangu mwaka 2018.

Misri yawa ya kwanza kuwa na mgonjwa wa Corona Afrika
RC Kilimanjaro azuia mshahara wa Mkurugenzi