Kiongozi wa chama kikubwa cha kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi ametangaza kujiondoa katika muungano wa vyama vya upinzani uliokuwa na lengo la kusimamisha mgombea mmoja kutoka upinzani katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika desemba 23 mwaka huu.

Kiongozi huyo wa chama cha Union for Democracy and Social Progress alitoa tangazo hilo siku moja baada ya makuabaliano hayo kutangazwa huko nchini Uswis barani Ulaya.

Aidha, viongozi saba wa upinzani, waliokutana huko Uswizi siku ya Jumapili, walimchagua mbunge asiye na umaarufu Martin Fayulu kuwa mgombea wao.

“Ninasema kuwa makubaliano yaliyoafikiwa Geneva hayajakubaliwa ndani ya vyama na yalikataliwa, Kutokana na hilo, ninaondoa uungwaji mkono wangu kutoka kwa makubaliano hayo, tuliyoyasaini,” amesema Tshisekedi wakati wa mahojiano na kituo cha radio cha Top Congo

Kiongozi mwingine wa upinzani, Vital Kamerhe pia alijitoa kwenye makubaliano hayo akisema hakukuwa na uungwaji mkono wa kutosha kutoka ndani ya vyama baina ya wanachama.

Hata hivyo, Chama tawala kimemchagua, Emmanuel Ramazani Shadary, aliyekuwa msaidizi wa zamani wa Rais Joseph Kabila kuwa mgombea.

 

 

 

Mwanamke aliyejioa nchini Uganda atimiza malengo yake
Rayvany afunguka kuhusu wimbo wake wa Mwanza