Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha inamshikilia Muweka hazina wa kikundi cha ujasiriamali cha Imani kwa tuhuma za kutafuna Tsh.Million 39 za Wanakikundi na kudai zimeyeyuka kwenye kibubu kwa imani za kishirikina.

Wiki iliyopita, tamu ya kugawana faida katika kikundi cha ujasiriamali cha Imani Mkoani Arusha iliingia doa baada ya baadhi yao kuzimia ghafla ukumbini kutokana na taarifa ya upotevu wa zaidi ya milioni 39 zilizodaiwa kuyeyuka kwa njia ya kishirikina.

Fedha hizo zinadaiwa ziliyeyuka ndani ya sanduku la fedha nyumbani kwa muweka hazina wa kikundi hicho chenye wanachama 20.

Mmoja wa wanakikundi, Grece Magala alisema kikundi chao chenye miaka mitano tangu kuanzishwa hawajawahi kugawana faida yoyote hadi siku hiyo walipokaa na kukubaliana kugawana faida iliyopo.

baada ya mkasa huo walikesha wakilia nyumbami kwa Muweka hazina huyo Halima Mwidadi Mkazi wa Osunyai Arusha.

Wengine waliokamatwa na TAKUKURU ni Katibu wa Kikundi Deogratius Seif na Mwenyekiti wake Aisha Saidi ambao walikamatwa jana na kuachiwa kwa dhamana huku Muweka hazina akiendelea kusota Mahabusu kwa sababu za kiupelelezi.

IGP Sirro "Tunamsubiri Lissu aje afungue kesi"
Heche na Mchungaji Msigwa wajisalimisha