Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha, katika Mikoa 9 hapa nchini, ikiwemo Dar es salaam, Pwani, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba huku Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe na Iringa mvua za masika zitaendelea kunyesha.

Taarifa hiyo imeeleza “Tahadhari ya vipindi vifupi vya mvua kubwa kwa maeneo machache ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe inaendelea”

Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia kuwepo kwa uwezekano wa kutokea Vimbunga pacha, muda wowote kuanzia leo Disemba 6, 2019, katika ukanda wa Bahari ya Hindi kutokana na kuwepo kwa migandamizo midogo ya hewa.

Aidha mamlaka hiyo imewashauri wananchi, kufuatilia taarifa za utabiri kutoka katika Mamlaka hiyo na kuzingatia tahadhari zinazotolewa.

Mbinu ya kugeuza kuku wa kisasa kama wakienyeji yafichuliwa
VIDEO: Vigingi uenyekiti wa Mbowe Chadema, Ma RC mtegoni