Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha Wilayani Chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji, kufuatia mvua.

Mvua hizo zimenyesha katika vijiji vya Olboloti ,Kaloleni na Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuathiriwa zaidi na mafuriko hayo, na kwamba shughuli za uokozi zinaendelea.

Mwenyekiti wa kijiji cha Olboloti, Abdallah Suti amesema mvua iliyonyesha katika maeneo yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya hiyo, Simon Odunga amesema kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni eneo hatarishi kwani wanazungukwa na milima huku akiwataka wananchi waliojenga katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja.

 

UVCCM yawajibu BAVICHA shambulio la JPM
Magazeti ya Tanzania leo Januari 12, 2018