Mvulana mmoja, Noble Uzuchi (17), anashikiliwa na  Kamandi ya Polisi ya Jimbo la Rivers nchini Nigeria kwa kuwapa ujauzito wanawake 10, sambamba na washukiwa wengine wanne wanaojihusisha na operesheni haramu ya uuzaji wa Watoto.

Kwa mujibu wa  chombo cha habari cha Nigeria, PUNCH, kimeripoti kuwa Kamandi ya Polisi ya Jimbo la Rivers nchini Nigeria ilifichua na kuzima operesheni ya biashara ya watoto katika maeneo ya serikali ya mitaa ya Obio/Akpor na Ikwerre jimboni humo.

PUNCH inasema, Kulingana na Afisa wa Polisi, Uzuchi na Chigozie Ogbonna (29), Kijana Ozuchi wliajiriwa na wamiliki wa biashara hiyo, ili kuwapa ujauzito wanawake hao kupitia ngono ya marathon, na tayari wajawazito hao wameokolewa.

Wanawake 10 baadhi yao wakiwa na watoto, wanaodaiwa kupewa mimba na kijana Noble Uzuchi (17). Picha ya PUNCH.

Kiongozi wa biashara hiyo, Peace Alikoi (40), anadaiwa kuwa hula fadhi watoto na kuwalipa akina mama kiasi cha Naira 500,000 na baadhi ya watoto wachanga pia waliuzwa, huku Polisi pia wakimkamata Favour Bright (30), kuhusiana na operesheni hiyo.

Taarifa hii imethibitishwa na Msemaji wa Polisi wa eneo hilo, Mrakibu wa Polisi Grace Iringe-Koko, alisema kupitia taarifa yake wakati akifanya kazi kwa mujibu wa taarifa za kijasusi zinazopatikana kwa Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Rivers, baada ya askari wa Kitengo cha Ujasusi cha C4I walipowavamia watu wawili.

Vikao vya Kikatiba, Dkt. Mwinyi awasili Dar
Lisu ataja tarehe ya kurejea nchini