Mvutano mkubwa umeanza kuonekana kwenye mitandao ya kijamii na kugeuka gumzo kati ya mashabiki wa wakali wa Bongo Flava, Diamond Platinumz na Mr. Blue kuhusu matumzi ya jina ‘Simba’ kati ya wasanii hao.
Gumzo hilo lilianza baada ya Mr. Blue kudai kuwa yeye ndiye aliyeanza kutumia jina ‘Simba’ (ambalo limeanza kutumiwa na Diamond hivi karibuni).
Gumzo linaloendelea mtandaoni kuhusu mvutano huo limepelekea baadhi ya akaunti maarufu kwenye mtandao wa Instagram kuanza kuwapigisha kura followers wao kuhusu nani ni Simba haswa.
Mbali na wasanii hao, msanii mkongwe Afande Sele aliwahi kutumia jina la ‘Simba’ akijiita ‘Simba Dume’.