Kiungo kutoka nchini Ureno João Mário Naval da Costa Eduardo, anakaribia kuihama klabu ya Sporting Clube de Portugal baada ya kuripotiwa aliwasili mjini Milan tayari kwa kujiunga na klabu ya Inter Milan ya nchini Italia.

Dili la usajili wa Mario kuelekea Inter Milan limekua na mshawasha mkubwa tangu klabu hiyo ilipomtangaza Frank de Boer kuwa mkuu wa benchi la ufundi juma lililopita.

Kituo cha Sky Sports Italia kimeripoti kuwa, Mario huenda akafanyiwa vipimo vya afya yake hii leo, kabla ya kukamilisha mipango mingine ya usajili klabuni hapo.

Hata hivyo kuna mashaka ambayo yamegubika suala la usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, kufuatia taarifa kudai kwamba bado kuna maelewano hafifu baina ya klabu ya Inter Milan na Sporting Clube de Portugal, kuhusu suala la ada ya usajili wa Mario.

Mario alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kilichotwaa ubingwa wa fainali za Euro 2016, baada ya kuwachapa waliokua wenyeji wa fainali hizo timu ya taifa ya Ufaransa bao moja kwa sifuri.

Drinkwater Awagomea Leicester City, Spurs Wachekelea
Bilic: Diego Costa Alistahili Kadi Nyekundu