Jana ilikuwa siku ya kihistoria nchini Canada baada ya chama cha upinzani cha Liberal kushinda katika uchaguzi mkuu na kukiondoa madarakani chama tawala cha Conservative kilichokaa madarakani kwa takribani Muongo mmoja chini ya aliyekuwa waziri Mkuu, Stephen Harper.

Justin Trudeau wa Liberal alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo huku Stephen Harper akimpongeza mapema na kuachia ofisi kwa kiongozi huyo mteule mwenye umri wa miaka 43.

Awali, tafiti mbalimbali zilikipa nafasi ya tatu chama cha Liberal na kukipa nafasi zaidi ya ushindi chama tawala hali iliyobadilika dakika za mwisho.

Kiongozi huyo mpya wa Canada ametangaza kuanza rasmi kazi yake akiahidi kuongeza kodi zaidi kwa matajiri ili kuongeza pato la taifa hilo.

Ushindi huo unakuja ikiwa ni miongo minne baada ya rais wa zamani wa Marekani, Richard Nixon kutabiri kuwa siku moja familia ya Trudeau itaiongoza Canada, hivyo, Justin anatarajiwa kuendeleza kazi ya baba yake Pierre Trudeau aliyewahi kuwa waziri Mkuu aliyejizolea umaarufu na heshima kubwa katika historia ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa BBC, ushindi wa Justin umechangiwa pia na kampeni kubwa iliyoendeshwa kwenye mitandao ya kijamii hasa na wanawake waliokuwa wakimpigia debe kwa madai kuwa ni mzuri na rais mwenye mvuto kuliko marais wote duniani (sexiest leader in the world).

 

Graham Poll Ayakubali Mabao Ya Arsenal
Rais Wa Syria Afanya Ziara Ya Ghafla Urusi Huku Ndege Za Marekani Zikielekea Kwake