Mlinda mlango  wa Azam FC, Mwadini Ally, ameongeza mkataba  wa mwaka mmoja ili kuweza kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Baada ya Ally kuongeza mkataba huo  amefanya idadi ya wachezaji waliosaini kandarasi mpya ya kuendelea kuitumikia Azam fc kuongezeka ambapo baadhi ya wachezaji ambao wamesha saini mkataba mpya ni mshambuliaji Donald Ngoma mabeki ni David Mwantika, Bruce Kangwa pamoja na Abdallah Kheri .

Kipa huyo alianza kuitumikia Azam FC tangu mwaka 2011 akitokea Mafunzo ya visiwani Zanzibar, amesaini mkataba chini ya usimamizi wa Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin na Mratibu wa timu hiyo Phillip Alando.

Uongozi wa Azam FC chini ya Amini kwakushirikiana na benchi la ufundi, wapo katika mchakato wa zoezi la kuwabakiza wachezaji waliomaliza mkataba pamoja na usajili wa wachezaji wapya kwa lengo la kuongeza nguvu  kwenye kikosi kwaajili ya msimu ujao.

Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo mapumzikoni na kinatarajia kurejea mazoezini Juni 20 mwaka huu, tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya 2019/2020 kwa kuanza na kibarua cha kutetea Kombe la Kagame CECAFA Kagame Cup kuanzia Julai 6 mwaka huu jijini Kigali, Rwanda.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 9, 2019
R Kelly akabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela