Mlinda mlango wa Azam FC Mwadini Ally, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa timu hiyo kwa mwezi Machi.

Mwadini ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kuwa na kiwango kizuri mwezi huo akicheza jumla ya michezo minne (sawa na dakika 360) akiruhusu wavu wake kutikiswa mara moja pekee.

“Kipa huyo amevuna asilimia 52 za kura 1,000 zilizopigwa na mashabiki wa soka kwenye ukurasa wa mtandao wetu wa facebook, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amevuna asilimia 25 huku Frank Domayo ‘Chumvi’ naye akivuna asilimia 23 ya kura hizo,” imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa kipa huyo mzaliwa wa kisiwani Unguja, visiwani Zanzibar kubeba tuzo hiyo, ambapo hadi hivi sasa wengine waliotwaa msimu huu ni Yakubu Mohammed, Mbaraka Yusuph, Himid Mao ‘Ninja’, Razak Abalora na Yahya Zayd.

Uongozi wa Azam FC umempongeza Mwadini kwa kutwaa tuzo na mashabiki wote walioshiriki kupiga kura.

 

Michael Carrick kuiongoza Man Utd
Kiongozi wa matawi Young Africans aishutumu TFF