Uongozi wa Klabu ya Young Africans umekiri kikosi chao hakikuwa na maandalizi mazuri, kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Siri ya kutokujiandaa vyema imelazimika kutolewa, baada ya kikosi cha Young Africans kukubali kupoteza nyumbani jijini Dar es salaam kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria kwenye uwanja wa Mkapa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amejitoa muhanga kutoa siri hiyo, baada ya kuwa sehemu ya viongozi waliopata fursa ya kuingia Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo huo ulioanza mishale ya saa kumi na moja jioni.

Mwakalebela amesema kwa hakika kikosi chao kilikua na maandalizi duni kabla ya mchezo wa jana Jumapili (Septemba 12), na ndio maana walishindwa kufanikisha lengo la kupata ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Amesema baada ya matokeo hayo, benchi lao la ufundi chini ya kocha Mkuu Nasridee Nabi litafanya kazi ya kurekebisha makosa yaliyojitokeza, ili kujiweka vizuri kabla ya mchezo wa mkondo wa pili utakaounguruma Jumapili (Septemba 19), Uwanja wa Yakubu Gowon, mjini Port Harcourt katika jimbo la Rivers.

“Tumepoteza mchezo nyumbani, tunakiri maandalizi yetu ya pre season hayakuwa mazuri, ni kama hayakuepo ila tunajipanga,” amesema Mwakalebela.

Kocha Nabi aliwahi kubainisha kuwa hajapata muda wa kutosha kwenye maandalizi ya timu yake iliporejea nchini ikitokea Morocco ilipoweka kambi ya muda mfupi ikiwa ni siku kadhaa kabla ya mchezo wa kimataifa wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zanaco FC Zambia, ambao pia Young Africans ilipoteza kwenye uwanja wa Mkapa.

Kocha wa Horseed FC aikubali Azam FC
Senzo kutangulia Nigeria, hofu yatawala