Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Fredrick Lameck Wilfred Lugano Mwakalebela ameanza tambo kuelekea Desemba 11, ambapo kikosi chao kitaalikwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Mwakalebela ametema tambo kuelekea mchezo huo, huku akiitaka Simba SC kujiandaa kwa kichapo kitakatifu ambacho kitaiheshimisha Young Africans msimu huu 2021/22.

Kiongozi huyo amesema wana kikosi kizuri na chenye kila sifa ya kupambana na yoyote msimu huu, hivyo Watani zao wa Jadi Simba SC itakiona cha moto.

“Yaani hao Simba SC wazionee hizo hizo timu nyingine lakini kwa Yanga lazima wakae.”

“Hawatuwezi kwa lolote, iwe kiwango uwanjani na nje ya uwanja tuko vizuri, sasa waje uwanjani hiyo siku hiyo tuko tayari kwa mapambano na watakiona cha moto.” Amesema Mwakalebela

Simba SC inatarajia kuanza maandalizi ya kuelekea mchezo huo wa Desemba 11, baada ya kuwasili jijini Dar es salaam ikitokea Lusaka-Zambia ilipokuwa kwenye Mchezo wa Mkondo wa Pili wa Kombe la Shirikisho hatua ya mtoano dhidi ya Red Arrows.

Mchezo huo uliochezwa jana Jumapili (Desemba 05), Simba SC ilipoteza kwa kufungwa 2-1, lakini imefuzu hatua ya Makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2.

Try Again: Tuna timu ya kumfunga yoyote
Simba SC yatangaza viingilio Desemba 11