Makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Fredrik Mwakelebela ameuponda mpango wa klabu ya Simba SC wa kuanzisha na kuendesha michuano ya Simba Super Cup, iliyoanzishwa rasmi mwaka huu 2021.

Michuano ya Simba Super Cup ilifikia tamati mwishoni mwa juma lililopita kwa michezo mitatu kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, huku Wenyeji Simba SC wakitawazwa kuwa mabingwa, baada ya kushinda mchezo mmoja na kuambulia sare mchezo mmoha, huku Al Hilal wakishinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja na TP Mazembe wakitoka sare mmoja na kupoteza mmoja.

Akizungumza na Dar24 Media Mwakelebela amesema uongozi wa klabu ya Simba ulipaswa kujipanga na kujitafakari kabla ya kuitangaza michuano ya hiyo, huku akipinga utaratibu wa utoaji wa zawadi ambazo kwa asilimia 100 zilikwenda Simba SC.

“Ninakubali kwamba wameandaa Simba Super Cup ila ilibidi wajipange na kufanya tathimini wakati mwingine, yaani umechukua kombe mwenyewe, kombe umeliaandaa mwenyewe.

“Upande wa tuzo binafsi nazo pia unajipa mwenyewe kuanzia mchezaji bora wako, mfungaji bora tena mabao yenyewe mawili, haikuwa inahitajika hiyo iwepo.

“Wajifunze baadaye kwamba sio lazima kuipa timu yako kipaumbele katika mambo ambayo umeyaandaa kisa wewe ni muadaaji.” Amesema Mwakalebela

Simba SC wameitumia michuano yaSimba Super Cup kama maandalizi ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya makundi, itakayoanza rasmi Februari 12, ambapo wawakilishi hao wa Tanzania wataanzia DR Congo kucheza dhidi ya AS Vita Club, kisha wataikaribisha Al Ahly kutoka Misri baadae mwezi huu.

Amshambulia mama mjamzito kwa bakora
Biden atangaza muelekeo mpya siasa za Marekani