Baada ya kushindwa kupanda daraja na kuwa sehemu ya timu za Ligi Kuu Msimu ujao 2021-22, Kocha Mkuu wa Pamba FC ya Mwanza Ulimboka Mwakingwe ametoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kupambana.

Pamba FC jana Jumamosi (Julai 24) ilipoteza mchezo wa hatua ya mtoano (Play Off) dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Taifa kwa kufungwa mabao 3-1.

Mwakingwe ambaye anakumbukwa kwa machachari yake alipokua mchezaji wa Mabingwa wa Tanzania Bara amesema: “Japokuwa hatujapata nafasi ya kucheza ligi kuu lakini nawapongeza wachezaji wangu sana kwa kujitolea na kufata maelekezo tuliyowapa lakini mpira ni mchezo wa wazi kilichotokea Tanga kila mtu ameona”

“Binafsi siwadai wachezaji wangu kwa lolote wamevuja jasho lao kulinda heshima Yangu na nembo ya Klabu ya Pamba fc pamoja na wana Mwanza”

Pamba FC imeshindwa kufikia lengo la kupanda Ligi Kuu kwa kufungwa jumla ya mabao 5-3. Baada ya kukubali sare ya 2-2 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa jijini Mwanza Jumatano (Julai 21).

Said El Maamry afariki dunia, kuzikwa leo Dar
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 25, 2021