Kufuatia kuvuja kwa video isiyo na maadili katika mitandao ya kijamii, iliyoleta gumzo kubwa mitandaoni ikiwaonesha wasanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Nandy na Bill Nas wakiwa faragha, wadau mbalimbali wameitaka Wizara husika kuwachukulia hatua stahiki wasanii hao ili iwe fundisho kwa wengine.

Mmoja ya wadau ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mshauri wa masuala mbalimbali ya mahusiano Dr. Chris Mauki amefunguka na kusema haya kufuatia sakata hilo.

“Mheshimiwa waziri Mwakyembe, Naibu Waziri pamoja na baraza la sanaa chini ya ndugu Mwingereza. Tutaiona nia yenu ya dhati kabisa kwenye kudumisha maadili na nidhamu katika jamii na hususani kwa wasanii ambao wanajiita “kioo cha jamii” pale ambapo hamtoinyamazia hii hali ya kuanikwa mitandaoni matukio ambayo kiuhalisia yalihitaji privacy, ninasimama sehemu ya ndugu zao hao wahusika, sehemu ya wazazi wao, sehemu ya wadogo zao, na wengine wengi ambao waliwaona kama role models wao. Kulikoni majukwaani tuwaone kama vioo vya jamii na huku nyuma mitandaoni mnaiharibu kabisa ile picha mliyoichora machoni pa watanzania” .

Mauki amesema kuwa kama ilivyoenea katika jamii  basi ameasa pia ni vyema jamii ikatambua ni hatua gani za kinidhamu zimechukuliwa juu ya wasanii hao walioanika mambo yao ya chumbani hadharani.

Amesema kwa kufanya hivyo itakuwa onyo kwa wengine wenye fikra finyu na chafu kama hawa wanaohalalisha tabia za kingono mitandaoni.

”Masikio ya wenye akili na hekima yanasubiri kusikia kutoka kwenu viongozi wetu wenye mpini” amesisitiza Chris Mauki.

Hata Hivyo mara baada ya kuvuja kwa video hiyo Nandy alitumia ukurasa wake wa instagram kuwaomba radhi watanzania na Serikali, japokuwa anadai mpaka sasa hajui aliyevujisha video hiyo richa ya kukiri kuwa ni yeye ndiye aliyeichukua kupitia mtandao wa snapchat.

Boko Haram wateka wasichana 1000
NHIF: Tumejipanga kuandikisha watoto 1,000 kwa siku