Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amehoji uhalali wa wabunge wa upinzani kuendelea kulipwa posho na mishahara wakati huu wanapoingia na kuondoka Bungeni bila kushiriki shughuli za Bunge.

Wabunge wa Upinzani wameanza kutekeleza azimio lao la kususia vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson huku wakiwasilisha barua rasmi la kutaka kuwasilisha bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Naibu Spika huyo.

Mwakyembe aliomba muongozo na kunukuu baadhi ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ikiwa ni pamoja na Ibara ya 23, ibara ndogo ya kwanza na ya pili ya Katiba.

“Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya. Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki,” Mwakyembe alisoma sehemu hiyo ya sheria.

Alilitaka Bunge lifafanue kwa kuzingatia ibara hizo uhalali wa wabunge hao kuendelea kulipwa mishahara na posho kwa kusaini mahudhurio pekee.

Naibu Spika aliahidi kuyatolea uamuzi mapendekezo hayo baada ya kufanya mashauriano na Uongozi wa Bunge.

Shiza Kichuya Athibitisha Kuihama Mtibwa Sugar
kinondoni yatekeleza agizo la 10% kwa wanawake na vijana