Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe ameshangazwa na janja janja inayofanywa na kampuni ya Star Media Tanzania Limited kwa kukiuka masharti ya leseni waliyopewa ya kurusha maudhui ya chaneli za ndani na kuwalipisha.

Mwakyembe amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa mara baada ya kubainisha janja hizo zinazofanywa na kampuni hiyo kinyume na leseni yao.

Amewataka wananchi wanaoendelea kulipishwa chaneli hizo kufika TCRA na kutoa ushahidi huo kwani kampuni hiyo imewahi kutozwa faini ya shilingi Milioni 100 mara baada ya kubainika wakiwalipisha wananchi kutazama chaneli za ndani.

”Lakini Startimes nawashangaa sana kama wameingia huko na mkataba wao unakaribia kuisha na sitegemei serikali ya awamu ya tano kama unaweza kufanya mzaa mzaa huo” amesema Mwakyembe.

Hayo yameibuliwa leo wakati Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maswali na majibu ambapo waandishi wa habari waliibua uhujumu huo unaofanywa na kampuni hiyo kupitia king’amuzi chake cha Star Times.

Aidha leseni waliyopewa StarTimes inahusisha kuonyesha chaneli za ndani kwenye ving’amuzi vyao na hazipaswi kulipiwa.

Mwakyembe amesema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa visimbusi vyote vilivyokiuka masharti ya leseni ya urushaji wa maudhui yake kwa kuwalipisha watanzania kutazama chaneli za ndani.

Marekani, Paraguay, Costa Rica, Mexico zapigana vikumbo kwa Sampaoli
Samuel Eto’o aikacha Ufaransa, aibukia Qatar