Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dr. Harrison Mwakyembe amevunja na kufutilia mbali baraza la michezo nchini Tanzania.

Hii ni kufuatiwa na madai ya ufisadi yaliyofanywa na  rais pamoja na maafisa wengine wakuu wa shirikisho la soka.

Baraza hilo ambalo linahusika na usimamizi  wa michezo nchini linatuhumiwa kwa kukosa utendaji na nidhamu ya kazi kwa ulanguzi wa fedha.

Aidha Mwakyembe ameilalamikia baraza hilo kwa kukosa uadilifu na uweledi wa kazi na kuweka mbele maslahi binafsi yaliyochochea ufisadi katika baraza hilo, madai ambayo aliyekuwa katibu mkuu wa baraza hilo Mohammed Kiganja ameyakana.

“kwanza nataka kusema kwamba hakujakuwa na ufisadi katika baraza hilo.Ufisadi umeshamiri katika michezo kwa jumla. Na ninakubaliana na hilo.Iwapo utaenda katika uchaguzi wa vilabu vya soka kuanzia viwango vya Wilaya hadi kitaifa utaona matatizo haya”. amesema Kiganja.

Kuvunjwa kwa baraza hilo kunajiri wiki mbili tu baada ya rais na maafisa wengine wakuu wa shirikisho la soka kushtakiwa kwa ulanguzi wa fedha.

Jeshi la Magereza nchini laanza kujipanga na uchumi wa Viwanda
Arsene Wenger: Tutasajili Wachezaji Wenye Hadhi Kubwa