Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe ametahadharisha kuhusu misaada inayotolewa na nchi za Magharibi na masharti yake akiwataka wananchi kufunga mkanda inapobidi kuliko kukubali masharti hayo.

Akizungumza hivi karibuni jijini Mwanza na watumishi wa wizara hiyo jijini humo, Dk. Mwakyembe alisema kuwa ni afadhali watanzania wafunge mkanda hata wakubali kufa kuliko kuyapigia magoti mataifa ya nje yanayotoa masharti yaliyo kinyume na utamaduni wa Kitanzania.

“Ni bora tufe masikini kuliko kuendeshwa kwa hofu, wao wanataka watuendeshe tu, sisi vitu kama vya ushoga vinapaswa kupingwa vibaya na haiwezekani kabisa,” alisema Dk. Mwakyembe.

“Vitu kama vya ushoga ni vya hovyo na kama watanzania hatukubaliani navyo, hata maadili yetu yenyewe hayataki mambo kama hayo,” aliongeza.

Miaka michache iliyopita, Waziri Mkuu wa Uingereza, Donald Cameroon alisema hadharani kuwa nchi za Afrika zinazopinga ushoga zisipewe misaada na taifa lake. Kauli ambayo haikuzaa matunda baada ya nchi za bara la Afrika ikiwemo Tanzania kushikilia msimamo wa kupinga ushoga.

Kauli ya Dk. Mwakyembe imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) la Serikali ya Marekani kutangaza kuinyima Tanzania msaada wa shilingi trilioni 1.3 za kitanzania kwa kile walichokieleza kuwa ni kufanya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar pamoja na utekelezaji mbaya wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco apenya mahakamani
Golden State Warriors Wavunja Rekodi Ya Chicago Bulls