Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na  michezo nchini Tanzania, Dkt Harrison Mwakyembe asema msanii wa muziki wa HipHop Roma Mkatoliki hajatoroka nchi bali aliondoka kwa shughul zake .

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Devotha Minja, aliyehoji juu wa masanii huyo kuondoka nchini na serikali kukandamiza uhuru wake.

“..Mimi nataka mheshimiwa aniletee ushahidi kwamba Roma amekwenda Marekani kwa sababu ya serikali kandamizi, Hapana Roma amekwenda kwa hiari yake mwenyewe na  mimi nimeongea naye alitaka kurejea nchini lakini hili swala la corona ndo limemkwamisha kurejea ” amesema Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe amesema wanasiasa wanawajaza maneno yasiyo na uhakika wala ukweli wowote wananchi na vijana wanaofanya jitihada za kutafuta kipato.

Ikumbukwe kuwa msanii huyo wa HipHop kabla ya kwenda nchini Marekani aliwahi kutekwa na watu wasiojulikana na alirejea uraiani baada ya kukutwa akiwa ametelekezwa na watekaji baada ya siku takribani 3.

Mitihani kidato cha sita yaahirishwa, mlipuko wa Covid 19
Ruksa Askari kupiga tochi mafichoni

Comments

comments