Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Mbalamaziwa iliyopo mkoani Iringa, Roida Mbalwa amefariki dunia kwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa kwenye mkutano na kiongozi mmoja kutumia vibaya fedha za ujenzi.

Mume wa marehemu, Sharif Utenga amesema kuwa kiongozi huyo aliitisha mkutano wa hadhara kata ya Mbalamaziwa na wananchi kueleza kuchangishwa michango mingi.

”Ninachofahamu ni kwamba alikuja kiongozi flani akazungumza na wananchi wakasema michango imekuwa mingi, ndipo hapo wakaamua kwenda kumkagua Mwalimu Roida, na baada ya ukaguzi ilibainika kuwa kuna hasara takribani milioni 200,”amesema Utenga

Aidha, Utenga amesema kuwa mara kwa mara viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi wamekuwa wakienda shuleni hapo na kukagua ujenzi kwasababu majengo hayo yanatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge.

”Mke wamgu alikuwa akipata presha ya kazi kutoka kwa viongozi waliokuwa wakifika kukagua, walikuwa wakali na kumtuhumu kwa matumizi mabaya ya fedha, alikuwa akiwaambia waalimu wenzake kuwa ipo siku atakuja kujiua,”amesema Utenga

Hata hivyo, diwani wa Mbalamaziwa, Zubery Nyamolelo amesema kuwa mwalimu huyo hajawahi kutuhumiwa kwa lolote.

Maalim Seif alipuka, 'Hakuna wa kuniziba mdomo'
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 19, 2019