Wazazi wa mwanafunzi wa kike wa shule ya msingi nchini Kenya wameripoti kitendo cha udhalilishaji wa kingono wa mwanaye kinachodaiwa kufanywa na mwalimu wa shule ya Slope View Academy.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Citizen, wazazi hao wamesema kuwa mtoto wao mwenye umri wa miaka 15 anayesoma darasa la nane alianza kumshangaza ‘matroni’ ya shule hiyo kwa kulia bila kueleza kinachomliza.

“Tulipokea simu kutoka kwa matroni wa shule hiyo aliyetuambia kuwa mtoto analia, hataki kunyamaza lakini hasemi kilichomsibu. Tulipoenda nikazungumza naye akatueleza kuwa mwalimu amemnyanyasa kingono,” alisema mama wa mtoto huyo.

Alisema kuwa baada ya kupata ukweli wa kinachomsibu mtoto huyo, tayari mwalimu aliyehusika alikuwa amekimbia.

Kwa mujibu wa maelezo ya mama huyo, msichana huyo anakabiliwa na tatizo la kubwa la kiakili na anatakiwa kupata msaada wa kisaikolojia pamoja na kitabibu.

Tukio hilo limeripotiwa polisi na tayari msako dhidi ya mtuhumiwa umeanza.

Vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto vimezidi kuripotiwa kutoka mashuleni na majumbani huku Serikali na mashirika ya Kimataifa yakitoa wito kwa wazazi kuzungumza na watoto wao kwa uwazi ili kuwapa uhuru wa kuwaeleza kila kinachotokea dhidi yao.

 

 

Tanzania mwenyeji kombe la Kagame, Simba na Young Africans zapangwa kundi moja
Zaha aeleza sababu ya kwenda Ivory Coast