Taasisi ya kuzuaia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara inatarajia kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Masasi, Mwanaid Abdalah Mtaka kwa tuhuma za kutumia nyaraka za uongo na kujipatia fedha kiasi cha Shilingi 1,578,000.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Takukuru Mkoani humo, Stephen Mafipa , amesema kuwa Mtaka anakabiliwa na kosa la jinai kwa kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake kisha kujipatia kiasi hicho cha fedha jambo ambalo ni kinyume na sheria.

“Alitumia na kuwasilisha stakabadhi zenye kuonyesha alitumia jumla ya shilingi 1,578,000/= kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya shule ya Msingi Masasi, hukub akijua kwamba hakununua,”Amesema Mafipa.

Aidha, kitendo hicho kilimuwezesha mtuhumiwa kujipatia kiasi cha shilingi 1,578,000/= ambazo alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Kesi hiyo ya Jinai itafunguliwa katika mahakama ya wilaya Masasi, ikihusisha makosa ya kutumia nyaraka za Uongo, kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba.11 ya mwaka 2007,  pamoja na kosa la Ubadhirifu na ufujaji wa mali ya umma kinyume na kifungu cha 28 kifungu kidogo cha kwanzacha sheria hiyo namba 11 ya mwaka 2007.

Wananchi Wampongeza JPM kwa Kuwawezesha Kupitia MKURABITA
Video: Wakurugenzi wana haki ya kusimamia uchaguzi- Wakili Manyama