Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno amesema Jeshi hilo limemuachia kwa dhamana Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantole kwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake.

Mwalimu huyo aliyefahamika kwa jina la Jonson Rwekaza ambaye anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi wake wa darasa la saba ambapo malalamiko hayo yaliwasilishwa polisi kupitia kwa mama mzazi wa mtoto.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda Otieno amesemaq kuwa, “ni kweli tuhumza hizo zipo na tumezipokea, kuhusu huyo mwalimu kumpa mimba mwanafunzi wake, ila upelelezi kwa sasa unaendelea ili ushahidi ukishakamilika aweze kufikishwa mahakamani”.

Awali akizungumza na vyombo vya habari mkoani Kigoma, Mama Mzazi wa mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alielezwa kushangaa kwa mtuhumiwa kuachiwa kwa dhamana, wakati ni mhalifu na kuiomba Serikali imsaidie kupata haki yake.

Video: Jeshi lenye Nguvu na Tishio zaidi Duniani
Halmashauri ya Njombe yatekeleza agizo la Serikali kwa Wanawake